nov
06
2015

Minembwe : watoto wajeshi watoroka vikundi vyao, Gomino pamoja na Maï Maï

Watoto 7 waume kutokea katika vikundi vyeye kumiliki silaha, vinavyotumikia Tchakira, Masango, Rubibi  na Bijombo . Walijiripoti bila silaha kwenye Offisi ya MONUSCO pa Minembwe centa siku ya kwanza tarehe 02 Novemba 2015.

Wakiojiana kwa siri na mwanaripota wa Redio Tuungane Minembwe ndani ya Kempi,watoto hawa wenye Umri ya miaka chini ya 18 walitufahamisha kwamba,wa 6 kati yao walikuwa ndani ya kikundi la Gomino na umoja ndani ya kikundi la wa Mai Mai linalojulikana kwa Jina la Mahoro .

Vijana hawo wadogo walieeza kuchoka na Maisha ya pori nakuonyesha utashi wa kuendelesha shule.Wakiomba serkali pia kuwalindia usalama sababu walitoroka usiku.

Tufahamishe kwamba ,watoto hawo wajeshi wamesafirishwa jana Siku ya Tatu na ndege la Monusco hadi mjini Uvira.

Wamoja kati yawo walizungumuza na GHISLAIN Bafunyembaka mwana ripota wa RTM,Tuwasikilize.

Alemoyo Sahiriza

Langues: 
Genre journalistique: 
Thématiques: 

Partager