nov
06
2015

Uvira: Mtoto mumoja amepigwa risasi na wenziwe

Kijana KIDANI mwenye umri ya miaka chini na 17 ameaga dunia kwakupigwa risasi na wenzake ambawo walikuwa wakijifunza kutumia silaha ndani ya kikundi cha Gomino, kinachotumikia milimani mirefu ya Minembwe.

Kufwatana na duru za jamaa,marehemu alijielekeza kwa utashi wake kujiunga  ndani ya kundi lenye kumiliki silaha la GOMINO pa Bijombo siku ya tano iliyopita akafariki juma pili tarehe 01 Novemba wakati akijifunza utumizi wa silaha.

Wenzi wake walimufyaturia risasi Kichwani pasipo kujuwa.

Tujulishe kwamba mauti ya marehemu iliwasili leo hii siku ya Inne kwa vigumu nyumbani kwake pa Muzinda, kijiji kinachopatikana kwenye kilometa 5 na madegu centa.

Alemoyo Sahiriza

Langues: 
Genre journalistique: 
Thématiques: 

Partager